MAREKANI: Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo


Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Maudhui ya mkutano huo wa wiki mbili ni changamoto na fursa katika kufikia usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake na wasichana waishio vijijini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kamisheni hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema huu ni wakati muhimu kwa kuhakikisha madaraka na usawa unamfikia mwanamke na hususani wa Kijijjini ambaye amekuwa akisahaulika

Naye mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, UNWomen, Phumzile Mlambo-Ngucka amesema maudhui hayo yanazingatia ukweli kwamba kampeni nyingi za kumkwamua mwanamke na msichana zinaangazia zaidi wale waishio mijini.

“Kwa msing iwa kutokumuacha nyuma mtu yeyote ni kuhakikisha hakuna anayeachwa nje. Moja ya michango mikubwa zaidi ya kufanikisha ajenda 2030 ni kuondoa ukosefu wa usawa unaokabili wanawake na wasichana waishio vijijini, ” amesema Bi. Mlambo-Ngucka.

Wakati wa mkutano mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo vikwazo vinavyokabili wanawake wa vijijini na mwelekeo bora ili wajikwamue.

Zaidi ya washiirki 8000 watahudhuria wakiwakilisha mashirika zaidi ya 1200 ya kiraia. Halikadhalika viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na vijana.

Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post