Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara mmoja kiasi cha sh. Million 8.
Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi kwa utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi ya cheo cha Kaptein.
Wengine ni Emmanuel Michael (45) mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela (50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment