DAR ES SALAAM: Rais Magufuli atoa neno kifo cha Dkt. Kabourou

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kaburu na kusisitiza kuwa amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Dkt. Magufuli ametoa salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga baada ya kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Kabourou aliyekuwa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili Jijini Dar es Salaam kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi  07, 2018.
"Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kabourou kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Dkt. Walid Amani Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu",amesema Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja na salamu hizo Dkt. Magufuli ameiombea familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
NA ISMAEL MOHAMED - EATV
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post