DAR ES SALAAM: JOSEPH BUTIKU: UVCCM MLINDENI RAIS MAGUFULI

Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, ndugu  Joseph Butiku, amewaasa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na watanzania kwa ujumla kumlinda Mhe. Rais Magufuli dhidi ya maadui zake ambao walikuwa wakitawanya na kujinufaisha na rasilimali za taifa huku wakiwaacha watanzania kwenye dimbwi la umaskini.
Mzee Butiku ameyasema hayo leo Jumapili Machi 4, 2018, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akiwasilisha mada ya Uzalendo na Historia ya Taifa letu kwa Viongozi, ikiwa ni sehemu ya mafunzo maalumu ya uongozi kwaajili ya vijana wa umoja huo kwa ngazi ya kata, wilaya na mkoa inayoendelea jijini Dar es Salaam.
“Uamuzi wa Rais Magufuli wa kuhakikisha rasilimali za taifa letu haziendelei kunyonywa na wezi wa ndani na nje umemletea maadui wengi sana na nyinyi vijana mnayo dhamana kubwa ya kuhakikisha mnamlinda Rais wetu kufa na kupona” amesema Butiku.
Toka Rais Magufuli aingie madarakani na kuanza kusimamia rasilimali za nchi ili ziwanufaishe watanzania wote hasa maskini, kumekuwepo na vilio kutoka kwa wale ambao walikuwa wakinufaika na rasilimali hizo, huku wakifanya kila njia kuhakikisha wanakwamisha juhudi zake, jambo ambalo halijafanikiwa, na kwa mwenendo wa Rais Magufuli inaonekana dhahiri shahiri kuwa mipango ya kumkwamisha haitafainikiwa maana wananchi wengi wamekuwa wakimuunga mkono.
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post