WAANDISHI WA HABARI NCHINI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI.

Waandishi wa Habari wa Redio za kijamii Nchini, Wameashwa kuzingatia Maadili pindi wawapo katika Majukumu yao ya kazi. Wito huo umetolewa na BI ROSE HAJI MWALIM amabye ni Mkufunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi hao zaidi ya 50 kutoka Redio mbalimbali za Kijamii yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, ambapo wamepiga kambi katika Ukumbi wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoani Dodoma kwa siku nane mfululizo.

Akizungumza na Washiriki hao Bi Rose amesema Redio ni chombo muhimu cha kupashana Habari na hivyo Waandishi wa Habari wanatakiwa kusimamia Misingi ya Taaluma yao ili kuepuka Madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kukosa umakini na kupuuza kwa Misingi hiyo muhimu.
Ameongeza kuwa Redia inasikilizwa na watu wengi kwa wakati mmoja na bila kujali Mapungufu yao kama vile Walemavu wa Macho, Wasiojua Kusoma, Watoto wadogo na hata Wazee hivyo amewataka washiriki hao kuandaa  Habari zenye kuleta Maslahi na kupunguza Mihemko kwa Jamii.

Kwa upande wao Washiriki hao wamefurahishwa na Mafunzo hayo ambayo yatawaongezea Uwezo katika kukamilisha Majukumu yao na wameahidi kuzingatia na kuyafanyia kazi yale yote wanayoendelea kujifunza kwa kipindi cha Siku hizo Nane .
Wameahidi kuwa Mabalozi wazuri pindi wataporudi katika Vituo vyao vya kazi kwa kuwashirikisha na Waandishi wengine ambao hawakuwepo kwenye Mafunzo hayo.

Mafunzo kama haya yamekuwa yakileta mabadiliko makubwa ya kiutendaji kutokana na kufundisha Masuala Muhimu na Nyeti yanayohusu Tasnia hii muhimu ya Habari Tanzania Hasa ukizingatia Redio za Kijamii ndio muhimili wa Maendeleo ya Wanajamii hasa wa Vijijini.

Pamoja na kufundisha mambo ya kuzingatia Maadili, Mengine ni pamoja na Kuwashirikisha Wanawake katika kuandaa na kutangaza Vipindi vya Michezo, Kuzipa kipaumbele Habari za Eneo husika, Waandishi wa Habari Wanawake kujiepusha na Rushwa ya Ngono, Kuzingatia Utofauti wa Kijinsi pamoja na kutumia Vyanzo Sahihi vya Habari.
Mafunzo hayo yanategemea kumalizika siku ya 13-02-2018 ambayo ni Siku ya Redio Duniani.

Karim Faida.

Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post