UNESCO KUADHIMISHASIKU YA RADIO DUNIANI

Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani.  Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari  wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari.
Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo,  usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo.
Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni,   Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO  katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani.
Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio.
Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika  huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu  mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki.
Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya.  Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi.
Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika.  Si tu redio inatumika kubadilishana  Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika.
Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii.
Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini  ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO.
Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo.
Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii,  kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na  kuboresha uwezo wao katika kazi
Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post