KISARAWE WAONGEZA MIKAKATI YA UFAULU SHULENI

Wilaya ya Kisarawe imedhamiria kuongeza kiwango cha ufaulu kwa
wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kwa kuweka mikakati kabambe
itakayowezesha wanafunzi kuwa mahiri katika masomo pamoja na mitihani.
Hayo yamebainishwa na Mbunge wa jimbo la Kisarawe Selemani Jafo
katika sherehe ya kuwapongeza walimu wa shule za msingi wilayani Kisarawe iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya minaki.

Katika sherehe  hiyo, Jafo ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, amewapongeza walimu wa wilaya hiyo kwa kuongeza ufaulu na kwamba inahitajika mikakati mingi zaidi ili wanafunzi wawe mahiri kwenye
mitihani.

Hata hivyo amesema hali ya baadhi ya shule za Kisarawe kuwa miongoni mwa shule kumi za mwisho katika mitihani kwasasa imetoweka.

Aidha Jafo ametoa maelekezo ya ununuzi wa mtambo mkubwa wa kudurufu
mitihani ili suala la uchapishaji wa mitihani ya shule za msingi na sekondari
usiwe tatizo tena.

Jambo hilo limeleta faraja kubwa kwa walimu waliokuwepo katika
sherehe hiyo kwani itawezesha kufanyika kwa mitihani ya kujipima kwa urahisi
wilayani humo.

Mtambo huo mpya unatarajiwa kununuliwa ndani ya wiki hii kwa kuwa fedha zimeshapatikana kutokana na michango kutoka kwa wadau mbalimbali wanao endelea kuchangia kampeni ya “Ondoa Zero Kisarawe” Kampeni hii imeonyesha kuzaa matunda kwani idadi ya wanafunzi waliopata daraja la sifuri imepungua kutoka wanafunzi 457 hadi 256.

Pia wanafunzi waliopata daraja la kwanza hadi daraja la nne wameongezeka na kufikia 163 wakati hapo awali walikuwa chini ya wanafunzi 50.



Share:

No comments:

SIKILIZA JAMII FM

Blog Archive

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

HABARI KUU WIKI HII

WAENDESHA BLOG

Contact Form



Recent post