NA Gregory Millanzi.
Ikiwa leo ni Jumapili
ya tatu tangu tuuanze mwaka huu 2018, Simanzi
na vilio vimetawala katika familia ya mzee Sandali, kufuatia kifo cha binti
yake Maria Sandali, ambaye amefariki dunia alfajiri ya Januari 20 mwaka huu
katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ambako alikua akitibiwa
tatizo la Saratani ya Mifupa.
Hali ilikuwa ya huzuni
katika makaburi ya familia ya Mzee
Sandali, katika kijiji cha Chikundi, halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani
Mtwara, umati wa watu umekusanyika katika safari ya mwisho ya kuumpumzisha
mwili wa binti Maria Sandali.
Marehemu Maria Sandali, wakati wa uhai wake akiwa nyumbani kwao kijiji cha Chikundi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara
Wazazi wa Marehemu
walikuwa na wakati mgumu sana kuamini kuwa hawatamuona tena Binti yao mpendwa Maria
Sandal, Mama mzazi wa Mariam bi Benardetha
Raymond na Baba yake Mzee Saidi Sandali, wameungana na wananchi pamoja na
wanafamilia wengine kuumsindikiza binti yao katika pumziko la milele, pia
wametoa pongezi kwa taasisi zote zilizojitolea kwa ajili ya matibabu ya mtoto
wao wakiwemo wizara ya Afya,hospitali ya Muhimbili(MOI) na Ocean Road.
Msiba huu umegusa
hisia za watu wengi kutoka maeneo mbalimbali wilayani Masasi, pamoja na
viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Masasi Selemani Mzee
aliyeambatana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Masasi Changwa Mkwazu, walihudhuria
mazishi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee(mwenye kaunda suti ya bluu) aliyeambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Changwa Mkwazu(mwenye mtandio wa njano) wakiwa kwenye makaburi ya Familia wakimsindikiza Marehemu Maria Sandal kwenye nyumba yake ya milele.
Awali, afisa mtendaji
wa kata ya Chikundi, Joseph Mtungulia, akaeleza wasifu wa marehemu kuwa baada
ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ndanda Masasi, waliandikiwa rufaa ya
nkwenda kutibiwa Muhimbili na ndipo Wizara ya Afya walichukua jukumu la kusimamia
matibabu ya Maria Sandali, mpaka mahuti yanamkuta tarehe 20 mwezi huu katika
Hospitali ya Ocean Road Dar Es Salaam.
Maria Sandali ambaye
alikua ni mwanafunzi katika shule ya sekondari ya King David Manispaa ya Mtwara
Mikindani alikuwa anasumbuliwa na uvimbe
kwenye bega kwa muda mrefu na baada ya kufanyiwa vipimo wiki iliyopita
akajulikana kuwa anatatizo la saratani ambayo ilikuwa imeshakuwa sugu,
Maria amefariki
dunia akiwa na umri wa miaka 17, Mungu ailaze roho ya
Marehemu Maria, mahali pema peponi aaamen.
…………………………………………mwisho………………………………………
No comments:
Post a Comment