SIMANZI NA MAJONZI VYATAWALA MAZISHI YA MARIA SANDALI, WILAYANI MASASI.
NA Gregory Millanzi.
Ikiwa leo ni Jumapili
ya tatu tangu tuuanze mwaka huu 2018, Simanzi
na vilio vimetawala katika familia ya mzee Sandali, kufuatia kifo cha binti
yake Maria Sandali, ambaye amefariki dunia alfajiri ya Januari 20 mwaka huu
katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ambako alikua akitibiwa
tatizo la Saratani ya Mifupa.
Hali ilikuwa ya huzuni
katika makaburi ya familia ya Mzee
Sandali, katika kijiji cha Chikundi, halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani
Mtwara, umati wa watu umekusanyika katika safari ya mwisho ya kuumpumzisha
mwili wa binti Maria Sandali.
Marehemu Maria Sandali, wakati wa uhai wake akiwa nyumbani kwao kijiji cha Chikundi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara
Wazazi wa Marehemu
walikuwa na wakati mgumu sana kuamini kuwa hawatamuona tena Binti yao mpendwa Maria
Sandal, Mama mzazi wa Mariam bi Benardetha
Raymond na Baba yake Mzee Saidi Sandali, wameungana na wananchi pamoja na
wanafamilia wengine kuumsindikiza binti yao katika pumziko la milele, pia
wametoa pongezi kwa taasisi zote zilizojitolea kwa ajili ya matibabu ya mtoto
wao wakiwemo wizara ya Afya,hospitali ya Muhimbili(MOI) na Ocean Road.
Msiba huu umegusa
hisia za watu wengi kutoka maeneo mbalimbali wilayani Masasi, pamoja na
viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Masasi Selemani Mzee
aliyeambatana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Masasi Changwa Mkwazu, walihudhuria
mazishi hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee(mwenye kaunda suti ya bluu) aliyeambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Changwa Mkwazu(mwenye mtandio wa njano) wakiwa kwenye makaburi ya Familia wakimsindikiza Marehemu Maria Sandal kwenye nyumba yake ya milele.
Awali, afisa mtendaji
wa kata ya Chikundi, Joseph Mtungulia, akaeleza wasifu wa marehemu kuwa baada
ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ndanda Masasi, waliandikiwa rufaa ya
nkwenda kutibiwa Muhimbili na ndipo Wizara ya Afya walichukua jukumu la kusimamia
matibabu ya Maria Sandali, mpaka mahuti yanamkuta tarehe 20 mwezi huu katika
Hospitali ya Ocean Road Dar Es Salaam.
Maria Sandali ambaye
alikua ni mwanafunzi katika shule ya sekondari ya King David Manispaa ya Mtwara
Mikindani alikuwa anasumbuliwa na uvimbe
kwenye bega kwa muda mrefu na baada ya kufanyiwa vipimo wiki iliyopita
akajulikana kuwa anatatizo la saratani ambayo ilikuwa imeshakuwa sugu,
Maria amefariki
dunia akiwa na umri wa miaka 17, Mungu ailaze roho ya
Marehemu Maria, mahali pema peponi aaamen.
…………………………………………mwisho………………………………………
TMA yatoa angalizo la mvua kubwa
Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo ya kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho Ijumaa.
Taarifa ya TMA imebainisha mikoa itakayokubwa na mvua hizo ni Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.
“Upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Hali ya Bahari, inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi na matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5,2018, kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.”
Hata hivyo, tayari mvua hizo zimekwisha kuanza na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani mvua ilinyesha jana Jumatano usiku katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.
Chanzo: mwananchi
WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
MAMLAKA YA HALI YA HEWA
S.L.P.3056, DAR-ES-SALAAM
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO
KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO
TAREHE:03/01/2018.
[Mikoa ya Rukwa, Iringa,
Mbeya, Njombe na Songwe]:
[Mikoa ya Dar es Salaam,
Pwani, Lindi na Mtwara]:
[Mikoa ya Kilimanjaro,
Arusha na Manyara]:
|
Hali ya Mawingu, mvua na
ngurumo katika baadhi ya Maeneo na vipindi vifupi vya jua.
|
||
[Mikoa ya Mwanza, Mara,
Geita, Shinyanga, Kagera na Simiyu]: [Mikoa ya Ruvuma, Kigoma, Tabora na
Katavi]:
|
Hali ya Mawingu kiasi, mvua
na ngurumo katika Maeneo machache na vipindi vya jua.
|
||
[Mikoa ya Tanga pamoja na
Visiwa vya Unguja na Pemba]:
[Mkoa wa Morogoro]:
|
|
Hali ya Mawingu, Mvua na
ngurumo katika Maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
|
ANGALIZO
VIPINDI
VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA DAR ES SALAAM, PWANI, ARUSHA,
KILIMANJARO, MANYARA, LINDI, IRINGA, MBEYA, SONGWE, NJOMBE NA MTWARA.
VIWANGO VYA JOTO, MAWIO NA MACHWEO YA JUA KWA BAADHI
YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI
|
Kiwango cha juu cha joto
|
Kiwango cha chini cha joto
|
Mawio (Saa)
|
Machweo (Saa)
|
ARUSHA
|
29°C
|
18°C
|
12:30
|
12:44
|
D'SALAAM
|
31°C
|
26°C
|
12:11
|
12:41
|
DODOMA
|
29°C
|
21°C
|
12:27
|
12:53
|
KIGOMA
|
29°C
|
19°C
|
12:53
|
01:15
|
MBEYA
|
25°C
|
16°C
|
12:31
|
01:07
|
IRINGA
|
24°C
|
19°C
|
12:24
|
12:56
|
NJOMBE
|
19°C
|
11°C
|
12:24
|
12:56
|
MWANZA
|
28°C
|
19°C
|
12:45
|
12:57
|
TABORA
|
28°C
|
19°C
|
12:41
|
01:03
|
TANGA |
29°C
|
20°C
|
12:16
|
12:38
|
ZANZIBAR
|
30°C
|
26°C
|
12:11
|
12:41
|
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvumakutoka Kaskazini;kwa kasi ya Km 30 kwa
saakwaPwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani
ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa Mawimbi
MadogohadiMakubwa kiasi.
Matazamio kwa siku ya Ijumaa:05/01/2018:
Kuongezeka kwa mvua katikaMwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za juu Kusini Magharibi.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 03/01/2018.
NA: MAMLAKA
YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 03 Januari, 2018 ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 03 Januari, 2018 ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Prof. Benno Ndulu Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo yao, Prof. Ndulu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kufanya nae kazi tangu alipoingia madarakani na amebainisha kuwa anafurahi kumaliza kipindi chake huku uchumi wa nchi ukiwa mzuri.
Prof. Ndulu amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa miongozo muhimu iliyosaidia kuimarisha uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei ambao mwezi Novemba 2017 ulifikia asilimia 4.4 na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.8 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 6 hivi sasa, hali ambayo imeimarisha uwezo wa Serikali kujiendesha na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.
“Nimekuja kumuaga Mhe. Rais na kumshukuru, nafurahi kuwa naondoka wakati hali ya uchumi ikiwa nzuri, Taifa linakopesheka na kuna mazingira mazuri zaidi ya uchumi kuendelea kukua, nampongeza sana Mhe. Rais kwa kusimamia mambo mbalimbali muhimu ya kuimarisha na kukuza uchumi katika kipindi chote nilichofanya nae kazi” amesema Prof. Ndulu.
Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Gavana Mteule Prof. Florens Luoga na baada ya mazungumzo hayo, Prof. Luoga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kumhakikishia kuwa ataisimamia BOT ili iendelee kuwa chombo imara cha kusimamia uchumi wa nchi, kuisimamia fedha ya Tanzania na kuhakikisha nchi inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).
Prof. Luoga ameungana na Prof. Ndulu kueleza kuwa taarifa zinazotolewa na BOT kuhusu ukuaji wa uchumi zinaandaliwa kitaalamu na kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na ameonya dhidi ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipotosha ukweli kuhusu takwimu za uchumi zinazotolewa na BOT.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Prof. Ndulu kwa utumishi wake wa miaka 10 na kazi nzuri aliyoifanya kusimamia uchumi ambapo katika kipindi hicho kasi ya ukuaji wa uchumi imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 5 hadi kufikia asilimia 7, ameimarisha usimamizi wa benki na maduka ya kubadilishia fedha, amesimamia ongezeko la akiba ya fedha za kigeni inayoiwezesha nchi kumudu kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi 6 na kuanza kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa reli, umeme, ununuzi wa ndege na mingine.
“Nakushukuru sana Prof. Ndulu, umefanya kazi nzuri ya kusimamia uchumi wa Taifa letu, ndio maana leo unamaliza muda wako lakini tayari Benki ya Dunia na kamisheni ya dunia inayoshughulikia teknolojia na maendeleo shirikishi wanakuhitaji ufanye nao kazi, na mimi nimeidhinisha uende ukatuwakilishe” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Gavana Mteule Prof. Luoga kwa kupokea uteuzi wake na amemtaka kufanya kazi ya kusimamia uchumi wa Taifa kwa ufanisi mkubwa zaidi ili nchi ipige hatua za maendeleo kwa kasi zaidi.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amesema mwezi ujao Serikali itatoa Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za Serikali, madai ya walimu na madai ya wakandarasi.
“Nasisitiza madeni tutakayolipa ni ya ndani, na tutalipa madeni ambayo yamehakikiwa, kwa hiyo maandalizi ya kutoa fedha hizo yaanze mara moja na ni matarajio yangu fedha hizi zitasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Januari, 2018